Home Lifestyle Nay Azungumzia Video Yake ya wimbo ‘Shika Adabu Yako’ kutochezwa kwenye Runinga

Nay Azungumzia Video Yake ya wimbo ‘Shika Adabu Yako’ kutochezwa kwenye Runinga

Msanii wa muziki wa Hip Hop, Nay wa Mitego amesema video yake mpya ya wimbo ‘Shika Adabu Yako’ kutochezwa kwenye runinga sio tatizo, kwani amedai tayari imeshafika pale alipohitaji ifike
Akizungumza na Bongo5 Jumatano hii, Nay alisema video hiyo ambayo audio yake ilifungiwa na Basata kutokana na kukiuka maadili, tayari imevunja rekodi za video za wasanii wa Hip hop zilizoangaliwa zaidi kwa muda mfupi kupitia youtube.
“Kuna baadhi ya TV kama tatu hivi nilisikia zilionyesha. Lakini hii video pia sikuisambaza kwenye TV niliiachia kwenye mitandao na bahati nzuri imeanya poa,” alisema Nay.

TRUE BOY
Aliongeza, “Unajua huu wimbo tayari Basata walishatoa taarifa kwamba ufungiwe lakini mimi sikupata taarifa rasmi. Kwa hiyo mimi sikutaka kuwadissapoint mashabiki wangu kwenye video, ndio maana video imeanza kuiachia youtube na bado inafanya poa tena huwenda ndio video iliyo ongoza kwa kuangaliwa kwenye youtube kwa wasanii wa Hip Hop. Kwa hiyo mimi naona nimefikia yale matarajio yangu kazi unaenda poa sana kwa sababu audio inafanya poa zaidi,”

Bongo5

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here