Home Lifestyle Ndoa ya DIAMOND na ZARI Inanukia?

Ndoa ya DIAMOND na ZARI Inanukia?

Sio kila mwanaume anapenda kumuita mpenzi wake ‘wife to be’ labda kama ameamua kuyatuliza macho yake kwa mwanamke mmoja tu kukubali kuwa muda wa na mwanamke mmoja maishani umefika. Kwa Diamond na Zari lakini wakiwa na mtoto mmoja na tayari na penzi likionekana kuota mizizi tayari, suala la wao kuhalalisha haliepukiki tena.
Na ndio maana ujumbe alioandika Diamond kwenye Instagram unaashiria kuwa huenda siku za wao kuwa Mr and Mrs Chibu rasmi zimekaribia. “A Morning Convo with My Beautiful Wife to be…. taking Blessings on what we about to do today…She always makes me Smile….Love you so Much Mama tee @ZaritheBossLady Nkwagara Nyo,” ameandika Diamond kwenye picha ya mazungumzo kwenye app ya Facetime.
Baraka anazozizungumzia Diamond kwenye ujumbe huo ni za utambulisho wa kitu kikubwa kutoka WCB ambacho licha ya mimi kuwa najua ni nini, kwa heshima na taadhima nawaachia wao wenyewe waumwage mchele muda ukifika. “Blessed to see another day, Stay tuned @wcb_wasafi is dropping a new hit today, you surely don’t wana miss this one,” ameandika Zari.

1 COMMENT

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here