Home Lifestyle “Nikiskia Jina La JAGUAR Nasikia KICHEFUCHEFU”- Asema PREZZO

“Nikiskia Jina La JAGUAR Nasikia KICHEFUCHEFU”- Asema PREZZO

Msanii Wa Humu Nchini PREZZO amesema akisikia jina la msanii mwenzake jaguar ambaye ni mhasimu wake mkubwa anasikia kichefuchefu.
PREZZO kupitia kipindi cha Strictly Kenya cha #EARADIO amesema anaamini kama mwanaume hatakiwi kumsema mwanaume mwenzake na JAGUAR alikuwa akifanya hivyo na kutumia jina lake kupata kiki.
KUHUSU KUMDHALILISHA MTANGAZAJI WA KTN.
Majuma kadhaa yaliyopita PREZZO alikumbana na Diss za kutosha kutoka kwa Watu mbalimbali baada ya kufanya interview na kituo kimoja cha Tv nchini Kenya na kufanya baadhi ya mambo yaliyotafsiriwa kama kumdhalilisha mwanadada mtangazaji live kwenye kipindi.

PREZZO amesema amerudia kuiangalia interview ile Mara 17 hadi akachoka na hakuona chochote kibaya alichokifanya kwa mtangazaji Huyo na pia mtangazaji huyo alimpigia simu baadaye kumuomba prezzo radhi hata hivyo taarifa za awali zilieleza kuwa mama yake prezzo alimpigia simu mwanadada huyo kumuomba msamaha kwa kitendo cha mwanaye. PREZZO yupo BONGO kushoot video na msanii mmoja wa Kenya na kufanya collabo kadhaa na wasanii wa BONGO .

PLANET DULLA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here