Home Lifestyle “Nimebadili style ya mavazi nina mchumba” – WOLPER

“Nimebadili style ya mavazi nina mchumba” – WOLPER

Msanii wa filamu nchini Tanzania, Jackline Wolper amesema kwamba kwa sasa yeye amebadili kabisa namna ya uvaaji tofauti kabisa na alivyokuwa akivaa zamani kutokana na kwamba kwa sasa ana mchumba hivyo inambidi kuvaa kiheshima zaidi. Akizungumza katika kipindi cha Nirvana kinachorushwa na EATV na kutangwazwa na Deogratius Kithama, Wolper ameweka bayana kwamba kwa sasa ana mchumba kutoka Kongo na mambo mengine kuhusu harusi yatajulikana hapo baadaye.
”Nimeacha kuvaa nguo nilizokuwa navaa awali kwa sababu nina mchumba hivyo napaswa kumheshimu na kuvaa kiheshima zaidi kuliko kuonyesha maungo kama zamani”- Amesema Wolper. Aidha kuhusu mambo ya urembo na utanashati usikose kutizama mwendelezo wa kipindi cha Nirvana jumanne saa tatu usiku ijayo ambapo Wolper atafunguka mambo mengi zaidi pamoja na kuonyesha pamba za uhakika anazomiliki.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here