Home Lifestyle “Nimetukanwa Sana Juu Ya Unene Wangu”- Peter Msechu

“Nimetukanwa Sana Juu Ya Unene Wangu”- Peter Msechu

Msanii wa muziki wa bongo fleva Peter Msechu amefunguka na kusema kuwa amekuwa akitukanwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu unene wake na kusema kuwa wapo baadhi ya watu walimfuata na kutaka kumpa dawa ili apunguze mwili wake.
Amesema licha ya kushawishiwa kwa hilo, yeye hataki kwa kuwa ameridhika na mwili huo. Akiwa katika kipindi cha Planet Bongo Peter Msechu amesema mwanzo alidhani kuwa ni yeye tu anatukanwa kwa sababu ya mwili wake lakini akagundua kuwa si yeye tu kwani hata msanii AT naye alikuwa anazungumzwa vibaya kutokana na wembamba wake.
“Unajua nilikuwa natukanwa sana kwenye mitandao ya jamii juu ya unene wangu, wengine walikuwa wananishauri hata nitumie dawa kupunguza mwili lakini nikagoma kwa sababu mimi nimeridhika na mwili wangu, sema nikawa najiuliza hawa watu wanataka nini maana hata watu wembamba wanasemwa kuwa wana UKIMWI na mambo mengine mengi tu’ Alisema Msechu. Mbali na hilo, Msechu amesema alipokuwa kwenye kituo kimoja cha Radio alimchana AT kuhusu wembamba wake, lakini AT hakupenda jambo hilo na kwamba hiyo ndiyo ilikuwa sababu ya AT kuandika ujumbe kwenye mitandao kumchamba Msechu, na kuongeza kuwa walipoona jambo hilo limekuwa kubwa ilibidi waligeuze kama fursa kwao ili wafanye kazi ya pamoja kuhusu mwili yao.
“Kuna siku nilimchana AT kwenye kituo cha Radio kumbe yeye hakupenda ndiyo akaandika ujumbe ule, mambo yakawa makubwa sana tukaona bora tuifanye fursa kwa kufanya wimbo wa pamoja’ alisema Peter Msechu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here