Home Lifestyle “Pete Ya Uchumba Sio Kigezo Kuwa Utaolewa” – Wolper

“Pete Ya Uchumba Sio Kigezo Kuwa Utaolewa” – Wolper

Wolper amefunguka hayo katika kipindi cha Nirvana kinachorushwa na EATV ambapo mtangazaji Deogratius Kithama alitaka kujua kwa undani kuhusu mwanadada huyo mrembo ni nani mchumba wake na yupo wapi kwa sasa.
”Mimi sipendi kuzungumzia masuala ya mahusiano yangu na mchumba wangu kwenye vyombo vya habari kwani huweza kutokea mtu akaishia kwenye ‘engagement ring’ hivyo nitasema nikashaolewa na sio sasa”- Amesisitiza Wolper. Aidha mwigizaji huyo ameweka wazi kwamba mchumba aliye naye kwa sasa alianza kumtongoza toka mwaka 2012 akakataa ila mambo yalivyoenda ndivyo sivyo kwa mchumba wa awali ikabidi amsikilize huyu ambaye yupo naye kwa sasa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here