Home Lifestyle PICHA: DIAMOND na P-SQUARE Washoot Video Nchini Afrika Kusini

PICHA: DIAMOND na P-SQUARE Washoot Video Nchini Afrika Kusini

P-Square walitawala vichwa vya habari kwenye redio, TV, magazeti na blogs za Afrika kwa kuingia kwenye vita vikubwa vya maneno kati yao kiasi cha kundi kudaiwa kuvunjika.
Peter hadi alianza kufanya show zake mwenyewe kwa jina la Mr P ikiwa ni pamoja na kuanzisha management yake baada ya kukataa kufanya kazi na kaka yake Jude Okoye. Paul naye tayari ana label yake mwenyewe, Rudeboy Records.

psquarewasafi
Na sasa huenda mambo yamerudi kawaida. Mapacha hao wapo Afrika Kusini walikoenda kushoot video ya wimbo walioshirikishwa na Diamond Platnumz. Wote kwa pamoja wamepost picha Instagram japo Diamond bado hajapost chochote. Mwanzoni wengi walidhani ni video yao wenyewe kabla ya Paul kupost picha mpya asubuhi ya leo akiwa amevaa kofia ya WCB na kuandika: It was great supporting a brother from east Africa ….. The king of east Africa, guess you already know who?”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here