Home Lifestyle Professor Jay Asema Atazidi Kufanya Mziki Hadi Afe.

Professor Jay Asema Atazidi Kufanya Mziki Hadi Afe.

Mbunge huyu wa eneo la  Mikumi amesema kwamba atafanya mziki hadi siku yake ya mwisho itakapo timia, hii ni baada ya Meneja Wa Diamond Platinumz Babu Tale kutaka kujua ni lini msanii huyo ataachia kazi nyingine.Babu Alisema kwamba mashairi ya msanii huyo humfurahisha sana kwa hiyo anatarajia kazi mpya toka kwake licha ya kusongwa na majukumu kadha wa kadha ya kuwahudumua wananchi.

PROFESSOR-JAY-22

“Nakushukuru sana Babutale kwa kuendelea kuniamini. Pia nimepata salaam nyingi za kunimiss kwenye game kutoka kwa mashabiki wangu wengi sana kutoka kona mbalimbali za dunia hii. Ni kweli kabisa kwamba kwa sasa nina majukumu makubwa sana ya kuwatumikia wananchi wenzangu wa jimbo la Mikumi lakini hilo halisababishi mimi kushindwa hata kwa uchache kuendelea kufanya muziki na kuwatendea haki mashabiki wangu wa ukweli walionibeba tangu siku ya kwanza mpaka sasa wanaendelea kuwa pamoja sana na mimi, ikumbukwe mimi ni mwanamuziki na nitaendelea kuwa mwanamuziki mpaka nione kibao kimeandikwa hakuna muziki”. Alisema Professor Jay.

Nakushukuru sana @babutale kwa kuendelea kuniamini, Pia nimepata salaam nyingi za kunimiss kwenye game kutoka kwa mashabiki wangu wengi sana kutoka kona mbalimbali za dunia hii, Ni kweli kabisa kwamba kwa sasa nina majukumu makubwa sana ya kuwatumikia wananchi wenzangu wa jimbo la MIKUMI lakini hilo halisababishi mimi kushindwa hata kwa uchache kuendelea kufanya Muziki na kuwatendea haki MASHABIKI wangu wa ukweli walionibeba tangu siku ya kwanza mpaka sasa wanaendelea kuwa pamoja sana na mimi, Ikumbukwe mimi ni mwanamuziki na nitaendelea kuwa mwanamuziki mpaka nione kibao kimeandikwa HAKUNA MUZIKI ? Muziki umenilea, Muziki umeendesha maisha yangu na Familia yangu, Muziki ndio ulionipa Heshima kubwa sana ulimwenguni, Bila MUZIKI leo Nisingekuwa MBUNGE WA MIKUMI, Nawaahidi mashabiki wangu wote mliokuwa mnaniuliza mara kwa mara kama nimeacha kufanya muziki kuwa Nitaendelea kufanya Muziki TILL I DIE, maana hiki ni kipaji cha Hali ya juu nilichopewa na Mungu kwa MAKUSUDI na kwa Upendeleo mkubwa na sio kwa bahati mbaya, NIMEWASIKIA na muda sio mrefu nitawatendea haki, ASANTENI sana kwa kuniamini nawapenda sana, Huu ni MGODI UNAOTEMBEA ? ? ? ? ? STAY BLESSED !!!

A photo posted by Professor Jay (@professorjaytz) on

Mwanamziki huyo pia aliongezea kwamba hawezi ushau mziki kwani ndio umemfungulia njia yake katika maisha ;

“Muziki umenilea, muziki umeendesha maisha yangu na familia yangu, muziki ndio ulionipa heshima kubwa sana ulimwenguni, bila muziki leo nisingekuwa mbunge wa Mikumi. Nawaahidi mashabiki wangu wote mliokuwa mnaniuliza mara kwa mara kama nimeacha kufanya muziki kuwa nitaendelea kufanya muziki till i die, maana hiki ni kipaji cha hali ya juu nilichopewa na Mungu kwa makusudi na kwa Upendeleo mkubwa na sio kwa bahati mbaya. Nimewasikia na muda sio mrefu nitawatendea haki, ahsanteni sana kwa kuniamini nawapenda sana, huu ni mgodi unaotembea” – Professor Jay

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here