Home Lifestyle “Sijaachia Ngoma Mpya Kama inavyoandikwa Kwenye Blogs”- STAMINA

“Sijaachia Ngoma Mpya Kama inavyoandikwa Kwenye Blogs”- STAMINA

Msanii wa bongo flava STAMINA SHORWEBWENZI ameweka wazi kuwa kwa sasa hana nyimbo mpya ambayo ameachia ila nyimbo ambayo ipo kwenye Mkito ilikuwepo kwenye album yake ya mwaka jana Mount Ulunguru, kupitia mtandao wake wa kijamii mkali huyo wa kuchana aliandika ” TANGAZO:sijaachia ngoma mpya kama inavyoandikwa kwenye blogs,,hiyo nyimbo iliyowekwa MKITO inaitwa BORA TUOANE ilikuwepo kwenye album yangu ya mwaka jana ya MOUNT ULUGURU na nilimshirikisha @kenny.kennie sio @bekaibrozama kama inavyoandikwa mitandaoni. ahsanteni” . STAMINA ni mmoja wa wasanii wa bongo flava wanaotabiriwa kutusua matawi ya juu mwaka huu wa 2017.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here