Home Lifestyle “Sijawahi Kuwa Na Mahusiano na Msanii” – Lady JayDee

“Sijawahi Kuwa Na Mahusiano na Msanii” – Lady JayDee

Mwanadada anayetamba kwa ngoma yake ya NdiNdiNdi Lady JayDee Amefunguka Kuwa kipindi chote ambacho anafanya muziki wa Bongo Flava hajawahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na msanii yeyote. JayDee ameyasema hayo alipokuwa akijibu maswali ya papo kwa papo wakati akizindua video ya NdiNdiNdi kwenye kipindi cha FNL kinachorushwa na EATV.
Katika uzinduzi huo msanii huyo aliweka bayana kwamba ameandaa album nzima ambapo ameanza kutoa single ya NdiNdiNdi na nyingine zitaendelea kutoka.
Aidha amewashukuru watu wote ambao wanaendelea kumuunga mkono katika kazi zake kwa muda mrefu sasa na kuahidi kwamba hatawaangusha.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here