Home Lifestyle “Sijawaongelea Joh na Nay Kwa Ubaya” – Chid Benz

“Sijawaongelea Joh na Nay Kwa Ubaya” – Chid Benz

Rapper Chid Benz alimaarufu kama Chuma amefunguka na kusema kuwa yeye hakuwaongelea Joh Makini na Nay wa Mitego kwa ubaya kuwa wanatengenezwa, bali watu wamemuelewa vibaya kutokana na kile alichokiongea. Chid Benz amesema hayo kwenye kipindi cha Planet bongo na kusema hakuwa na maana ya kuwa Joh Makini na Nay wa Mitego wanatengenezwa kwa kuwa hawana uwezo hapana bali alizungumza kuwa wasanii hao wana uwezo wao binafsi katika muziki.
“Watu wanachanganya na kunielewa tofauti katika kile nilichokisema, swala la Joh Makini na Nay wa Mitego sikuongelea kwa ubaya, sikuongelea sijui wao wanapewa kiki hawana uwezo ‘No’ sikusema hivyo nilizungumzia wasanii wengi kwa ujumla wanatengenezwa kwa namna fulani katika game, ambayo si mbaya kwani hata ulaya kuna wasanii wanatengenezwa, mfano hata kwa saizi hata mimi ninatengenezwa ni yale yale, sikusema kuwa wao wanatengenezwa hawana uwezo hapana, Joh Makini ana uwezo ndiyo maana hata anapata watu wa kumtengeneza kama yupo, Nay wa Mitego pia ana uwezo ndiyo maana anatengeneza muziki wake, ana mashabiki wake na anapata pesa sababu ana uwezo” alisema Chid Benz. Mbali na hilo Chid Benz alisema kuwa anaamini kuwa wasanii hao hawakumuelewa tofauti ila kama wataona kuwa amewazungumzia vibaya itakuwa bahati mbaya lakini yeye hakuwa na maana mbaya, kama inavyochukuliwa mtaani.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here