Home Lifestyle “Sijibishani Na Wasio Level Yangu”- NAY

“Sijibishani Na Wasio Level Yangu”- NAY

Rapper wa muziki nchini Tanzania, Nay wa Mitego, amesema kwa level aliyonayo kwenye game la muziki hawezi kushindana na msanii ambaye anatafuta kiki kupitia yeye na huku hafikii levo yake. Nay wa Mitego, aliyazungumza hayo Ijumaa kwenye kipindi cha Friday Night Live ya EATV na EA Radio baada ya kuulizwa kuhusiana na tetesi kwamba hapo awali alikuwa akitungiwa nyimbo na rapper Kimbunga Mchawi kisha anapoziimba Kimbunga hurejea kutunga nyimbo kwa ajili ya kumjibu Nay wa Mitego.
Nay wa Mitego amesema kuwa kwa sasa yeye yupo juu kimuziki hivyo hawezi kujibishana kuhusiana na msanii Kimbunga Mchawi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here