Home Lifestyle “Sina Mpango Wa Kuoa Leo Wala Kesho”- Dully Sykes

“Sina Mpango Wa Kuoa Leo Wala Kesho”- Dully Sykes

Msanii wa Bongo Flava Dully Sykes amefunguka kuwa hatafunga ndoa hivi karibuni, akiongea kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Dully amesema yeye kwake kuoa ni sawa na maji kufuata mkondo, kwana hata marehemu baba yake hakuwahi kuoa wakati wa uhai wake.
“Kila mtu ana mipango yake, maji hufuata mkondo, wewe nafikiri mzazi wako alioa, mi baba yangu hakuwahi kuoa”, alisikika Dully akielezea sababu ya yeye kutoamua kuoa mpaka leo. Pamoja na hayo Dully amesema akiona kuna umuhimu na ikiwezekana ataoa, hivyo amewataka wadau wake wamuombee ili aweze kuwa na mawazo ya kuoa na kuwa na mke rasmi.
“Kama inawezekana naweza kuvuta jiko, na kama haitowezekana sitavuta jiko, kwa sababu sijafikiria bado, mniombee nipate mawazo ya kuchukua jiko, sio kwa vile FA amefanya basi ndo uone inawezekana, nina sababu zangu tu mwenyewe, nikikwambia ntakuvunja moyo kama umeoa wewe”, alisema Dully Sykes.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here