Home Lifestyle Sina tatizo la Baraka Da Prince – Young Killer

Sina tatizo la Baraka Da Prince – Young Killer

Rapa Young Killer anayeiwakilisha Mwanza katika muziki wa Hip hop amefunguka na kusema kuwa yeye hana tatizo lolote na msanii mwenzake Baraka Da Prince ambaye anatokea Mwanza pia na kusema yeye ni shabiki wa msanii huyo kwa sababu anafanya kazi nzuri .
Young Killer anasema kwamba hata yeye kuna maneno aliyasikia lakini anaamini yeye hana tofauti yoyote na msanii huyo anamkubali kutokana na kazi yake nzuri anayofanya kwenye muziki wa bongo fleva .
Mbali na hilo Young Killer amesema kuwa kwa sasa ataendelea na utaratibu wake wa kutoa wimbo kila baada ya miezi mitatu na anafanya hivyo kutokana na ukweli kwamba wasanii wengi wanakuwa wanatoa ngoma hivyo anaona akikaa kimya itamfanya apotee kwenye game .

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here