Home Lifestyle “Sitaacha Kujipaka ‘Make Up’ Kwa Hofu Ya Watu” – Asema HEMEDY

“Sitaacha Kujipaka ‘Make Up’ Kwa Hofu Ya Watu” – Asema HEMEDY

Msanii wa Bongo Fleva Hemed Suleiman ‘Hemedy PhD’, amesema kwamba hataacha kutumia vipodozi kwa kuwa humuweka nadhifu na humwongezea mvuto wa mwili wake. Hemedy ambaye amewai kushiriki kwenye mashindano  alisema vipodozi anavyotumia zaidi ni powder, lipshine na perfume na hataacha kujiremba.
“Sitaacha kujiremba kwa sababu kujiremba siyo kwa wasichana tu hata wanaume tunatakiwa tujipake vipodozi, kama powder na lipshine zinasaidia kuongeza mvuto na mwonekano nadhifu zaidi, mimi ni star natakiwa niishi kistaa hivyo vipodozi ni kitu cha kawaida.
“Mara nyingi vipodozi navitumia nikiwa katika kazi zangu ili nionekane tofauti nyumbani na kazini hivyo nasisitiza kwamba siwezi kuacha kupaka vipodozi kwa kuogopa maneno ya watu,” alimaliza Hemedy.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here