Home Lifestyle “Sitaki Tena Kumweka Wazi Mpenzi Wangu”- LINAH

“Sitaki Tena Kumweka Wazi Mpenzi Wangu”- LINAH

Msanii Linah Sanga ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake ya mpya ‘Imani’ amefunguka na kusema kuwa kwa mambo ambayo tayari yamemkuta kwenye mahusiano hayupo tayari tena kumuweka wazi mpenzi wake kwenye mitandao ya kijamii. Linah Sanga akiongea kwenye kipindi cha Enews amesema kwamba kwa sasa yeye hayupo tayari kumuweka wazi mpenzi wake kama ilivyokuwa awali kwani jambo hilo kwanza linapelekea watu kuanza kufuatilia maisha yake ya mahusiano na si kazi zake za muziki. Mbali na hilo Linah Sanga amefunguka na kusema kuwa wapo watu kwenye mahusiano wanaingia ili kutaka kuonja penzi la mtu na kuona huyo mtu yupoje kwenye mapenzi ila hawana mipango endelevu wala hawaangalii mipango ya baadaye.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here