Home Lifestyle “Siwezi Kumtongoza Mtu Kwenye Instagram” – Shettah

“Siwezi Kumtongoza Mtu Kwenye Instagram” – Shettah

Msanii Shettah amesema kuwa yeye kama yeye hawezi kumtongoza mtu kwenye mitandao ya kijamii , wala kumuomba mtu pesa kwenye mitandao ya kijamii kwani yeye tayari anafamilia yake na maisha yake .
Shettah alisema haya kufuatia kuwepo kwa kijana ambaye anatumia mitandao ya kijamii na kutapeli watu kwa kutumia jina lake huku kijana huyo akisemekana anawatongoza wanawake kwenye mitandao hiyo yta kijamii akitumia jina la msanii huyo.
” Unajua kuendelea kukaa kimya kwa kitu ambacho kinalalamikiwa kila siku ni kufanya watu waamini kuwa huenda mtu huyo unashirikiana naye, yule kijana nimempost kwenye mitandao ya kijamii ili watu wajue kuwa mwizi wa mitandaoni ambaye alikuwa akitumia jina langu kuwatapeli watu pesa zao na kuwatongoza wanawake kwenye mitandao ya kijamii , watu wanatakiwa kuelewa kuwa mimi kama mimi siwezi kumuomba mtu pesa kwenye mitandao ya kijamii , wala siwezi kumtongoza mtu Instgram mimi nina familia yangu na maisha yangu hata kama ninaweza kufanya vitu hivyo lakini siwezi kufanya kwa njia hiyo ‘ alisema Shettah

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here