Home Lifestyle Siwezi Kutibiwa Na Mwanamke” – KHADIJA KOPA

Siwezi Kutibiwa Na Mwanamke” – KHADIJA KOPA

Malkia wa mipasho nchini Tanzania Khadija Kopa amefunguka sababu za yeye kuwapenda madaktari wa kiume kuliko wanawake na kusema kuwa mara nyingi wanawake wanakuwa hawawajali wanawake wenzao ukilinganisha na madaktari wanaume wanavyowapa huduma wanawake. Malkia Khadija Kopa aliyasema hayo kupitia kipindi cha Wanawake Live kinachorushwa na ting’a namba moja kwa vijana EATV ambapo yeye amekiri wazi kuwa mpaka leo akienda hospitali hataki kutibiwa na manesi wala madaktari wa kike kutokana na ukweli kwamba wanwake wengi hawapendani.
“Unajua wanawake mara nyingi wananyodo hicho ndio kitu ambacho mimi mpaka leo napenda kutibiwa na madaktari wanaume, yaani mimi sindano nataka kuchomwa na mwanaume, hata kuzalishwa siku zote mimi nazalishwa na madaktari wa kiume sababu wanawake hatupendani” alisema Khadja Kopa.
Lakini mbali na hilo Malkia huyo wa mipasho aliwasii wanawake kupendana wao kwa wao ili waweze kupiga hatua mbele zaidi na kusema kitendo cha kutopendana kinawakwamisha kupiga hatua kimaendeleo na kujenga chuki kati yao. “Unajua sisi wanawake hatupendani, mimi hapa ni mwanasiasa hivyo hata nikigombea nafasi fulani nitapata kura nyingi zaidi kutoka kwa wanaume na si wanawake, lakini ningependa leo niwaambie tu hata ukimkuta mwanamke wenzako anagombea nafasi fulani muoneshe support ya moja kwa moja, jamanii tunabidi tupendane” alisisitiza Khadija.

EATV

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here