Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo leo imetangaza kumfungia Snura kujihusisha na masuala ya Sanaa. Pia Wizara imeufungia wimbo wake #Chura pamoja na video yake kutochezwa kwenye Redio na TV nchini, taarifa hiyo imetolewa na Wizara hiyo kwenye mkutano na Waandishi wa habari uliofanyika kwenye ukumbi wake wa mikutano wizarani hapo jijini Dar mapema asubuhi ya leo. Agizo kwa wale watakaokiuka watashtakiwa kwa kutumia sheria ya makosa ya mtandao.