“Swala la Raymond Halitingishi”- Kamikaze

    Msanii wa Bongo Fleva kutoka katika kundi la Wakacha, Cyril Kamikaze, afunguka juu ya seke seke lake na msanii kutoka katika kundi la WCB Raymond baada ya uongozi huo kusema hawaitambui ngoma hiyo wakidai ametoa wimbo bila ya kuwashirikisha. Akizungumza na eNewz Kamikaze alisema kuwa ile ngoma ni mali yake na alishafanya mkataba na Raymond kuwa anaishikilia yeye hivyo WCB alitakiwa labda akaombe kumtumia msanii wao kufanyanaye video na siyo kuomba ngoma itoke.
    “Nimefanya ngoma na Raymond kabla hajajulikana na hivyo unaweza ukagundua mimi sitegemei jina la mtu kufanya ngoma nilipenda uwezo wake na nikaamua kufanyanaye kazi kwahiyo hata kama asingelikuwa amesainiwa sehemu yeyote duniani ningeliitoa tu hiyo ngoma,” alisema Kamikaze na kuongeza “Mimi nafanya mziki kwa kwa muda mrefu sana kwahiyo hakuna mtu yeyote anaeweza kunitingisha akaniambia lolote, sijui wanaweza wakasema wanataka kunitingisha kwenye kipi mimi naamini kwenye kazi nzuri suala la Raymond siyo kwamba linatingisha ngoma mimi kwanza nimetoa ngoma zangu nyingi bila ya kolabo”.

    LEAVE A REPLY

    Please enter your comment!
    Please enter your name here