Home Lifestyle ‘Sweet Love ilituchukua Siku Mbili Kurecord’ – AKOTHEE Amzungumzia Collabo Yake...

‘Sweet Love ilituchukua Siku Mbili Kurecord’ – AKOTHEE Amzungumzia Collabo Yake Na DIAMOND PLATNUMZ

Msanii Wa Kike Wa Humu Nchini AKOTHEE, Hivi Majuzi Aliachia Kazi Yake Mpya ambaye amemshirikisha gwiji wa Afrika Mashariki DIAMOND PLATNUMZ Inayokwenda Kwa Jina ‘Sweet Love’. Akizungumza na Mzazi Willy M TUVA Kupitia Kipindi Cha #MamboMseto Ya Radio Citizen, Msanii Huyo Alifunguka Kuwa Kazi Hiyo ilichukua siku mbili Kurecord “Sweet Love ilituchukua Siku Mbili Kurecord, Tulianza Kurecord Kwanzia Saa Tatu Usiku Hadi Saa Kumi Asubuhi Na Producer LIZA kwenye studio za WCB” Alisema Akothee. Kuhusu Swala La Hela Kama alimlipa Diamond Platnumz Kufanya Naye Kazi, Akothee alikuwa na Haya ya Kusema ” Muziki ni biashara, na kila mtu akifanya biashara lazima aone matokeo ama inaitwa profit ,na ngoma imetoka kwa ivyo tushughulikie audio na video. Swala La Hela Hilo tusiingilie, maanake mara nyingi nikitaja kitu tu watu wanakasirika wanaanza kusema mbona hakutumia hiyo sijui kuenda kufanya nini ” alimazia AKOTHEE.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here