Home Lifestyle “Ukiona Unakosa Cha Kuchekesha Watu Bora Utafute Kazi Nyingine Ya Kufanya”- BARAKAH...

“Ukiona Unakosa Cha Kuchekesha Watu Bora Utafute Kazi Nyingine Ya Kufanya”- BARAKAH DA PRINCE Kwa ERIC OMONDI

Msanii wa Bongo Flava BARAKAH DA PRINCE ambaye sasa hivi anafanya vizuri na kazi yake Mpya na TIMBULO ‘Usisahau’, ameonekana kugadhabishwa na tendo la mchekeshaji maarufu humu nchini ERIC OMONDI kupiga picha akiwa msalabani.

Msanii Huyo kupitia instagram aliandika “Ukiona unakosa cha kuchekesha watu bora utafute kazi nyingine ya kufanya kuliko alichofanya huyu sijui ndio anaitwa nan…kawakosea sana watu wote wenye imani ya kikristo…tafuta kazi nyingine… maana vichekesho nahisi umefikia mwisho…huyu jamaaa kafanya asubuhi yangu kuwa mbaya sana..shukuru wakristo ni wapole..ukifanya kitu ichi kwa Muslim..ungefanywa mfano “. Eric Omondi ambaye alikuwa ana tayarisha refix ya KULIKO JANA hajasema lolote kuhusiana na hilo swala.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here