Home Lifestyle Ukweli Kuhusu Mr.Blue Kumpigia Simu Demu Wa Baraka Da Prince. 

Ukweli Kuhusu Mr.Blue Kumpigia Simu Demu Wa Baraka Da Prince. 

Wiki iliyopita tulimsikia Mr Blue akizungumza kwenye U-Heard kuhusiana na tuhuma za yeye kumpigia simu ex girlfriend wake ambaye sasa ni mpenzi wa Baraka Da Prince afahamikae kama Naj, na kwa mujibu wa taarifa hizo inasemekana kuwa simu hiyo ilipokelewa na Baraka Da Prince.

Mr Blue alifunguka kuwa yeye hajui chochote kuhusiana na issue hiyo na wala hawezi kumpigia simu Naj kutokana na yeye sasa hivi ana mke wake. Ila kwa taarifa alizozipata za kunyapia nyapia ni kwamba skendo hiyo ni kiki ambayo imeandaliwa na kina Baraka Da Prince kutokana na wao wanataka kuachia nyimbo yao hivi karibuni, kwahiyo wanataka kuitumia hiyo kama kiki iliiweze kuwafikisha sehemu fulani ili ngoma yao iweze kupenya.

“Sina Bifu na Baraka na wala siwezi kuwa na Bifu na Baraka kwasababu siku zote Meli haiwezi kugongana na Bajaji,  yule namchukuliz kama mdogo wangu na siwezi kuwa na tatizo nae. Namshauri na ninampenda, kama yeye amefanya au kuna watu wamefanya naomba watoe prove kwa kuonyesha namba yangu kwenye mitandao” Yalikuwa ni maneno ya Mr Blue akisisitiza kuwa kama ni yeye amefanya hicho kitendo basi waionyeshe namba aliyotumia kupiga kwenye namba hiyo katika mitandao ndio itajulikana kama ni yeye au sio yeye.

Perfect255.com

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here