Home Lifestyle Ukweli Kuhusu Picha Ya Diamond Na Kanye!!

Ukweli Kuhusu Picha Ya Diamond Na Kanye!!

Diamond ameeleza kwa kina Tukio la kupiga picha na kanye west ambayo baada ya kuipost kuliibuka story nyingi kila mmoja akisema lake.

Akizungumza katika kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio,Diamond amesema hiyo ilikuwa alipoenda marekani wakiwa uwanja wa ndege kuelekea nje alitokea mtu ambaye hakumjua kwa kuwa alikuwa bize kuchat kwenye simu na alimuomba apige picha viatu vyake naye akamjibu bila kumwangalia vizuri “OK cool”.

Amesema baada ya kuona mtu huyo katumia Muda mrefu kufanya zoezi hilo ndipo alipoondoa macho yake kwenye simu kumuangalia huyo mtu kutaka kujua kitu gani kilifanya apige picha viatu vyake Muda mrefu kiasi hicho.

Ghafla alishtuka kumuona mtu Huyo alikuwa ni Kanye West na kuanzia hapo ndipo kujitambulisha kukawa kwingi sana akijaribu kutumia fursa hiyo kutengeneza link naye.

Anasema alishangazwa na jinsi Kanye alivyotoa ushirikiano.

Hata hivyo diamond ameficha kuhusu kile kilichoendelea kuhusu kufanya Kazi pamoja lakini amedokeza kuwa deal imekaa poa kwa zaidi ya 100%.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here