Ukweli Kuhusu ‘SKULL’ ofisini Kwa DIAMOND PLATNUMZ

  Kuna story Zilivuma mtandaoni na kuandikwa na baadhi ya magazeti ya udaku kuwa kuna ‘Skull’ ama Ukipenda fuvu la mtu mezani ofisini kwa DIAMOND PLATNUMZ jambo lililoibua hisia tofauti wengine wakilihusisha na imani za kishirikina. Meneja wa DIAMOND, BABU TALE amezungumza na #Planetbongo kuelezea ukweli kuhusu issue hiyo akishangazwa na jinsi watu walivyochukulia kuliona fuvu hilo. “Kwanza kabisa ukweli ni kuwa lile sio FUVU halisi la mtu kama wengi walivyosikia ila ni kito tu kilichotengenezwa mfano wa FUVU na Diamond aliliona nchini Sweden akalipenda na kuamua kuliweka kama pambo ofisini kwake” Alisema TALE.

  skul

  Kwa mujibu wa BABU TALE hakuna uhusiano wowote wa pambo hilo na ushirikina na ndiyo maana limewekwa sehemu ya wazi tu kila mtu anaweza kuliona ila watu waliovumisha hilo huenda wakawa na imani hizo lakini sio DIAMOND .
  TALE ametoa mifano ya watu wengi ambao huvaa #culture mikononi ambazo zina mafuvu ya kichwa au hata cheni ambazo huwa na urembo kama huo lakini haihusiani chochote na nguvu za giza. Alimalizia hata yeye alinunua baadhi ya vitu vya thamani kwaajili ya mapambo na Diamond Naye alinunua ikiwemo hicho ambacho watu wamegeuza kuwa story na kuhusianisha na ushirikina.

  LEAVE A REPLY

  Please enter your comment!
  Please enter your name here