Home Lifestyle “Unaweza Nichukia ila Ukapenda Muziki Wangu ” – Alikiba

“Unaweza Nichukia ila Ukapenda Muziki Wangu ” – Alikiba

Msanii Alikiba amefunguka na kusema kuwa muziki hauna siri na muziki hauna tofauti kati ya mtu na mtu kwani unaweza kuwa una chuki na yeye lakini akiimba muziki mzuri ukapenda kazi yake na kuimba. Alikiba alizidi kutoa ufafanuzi kuwa kama binadamu inawezekana ukatoa labda humpendi mtu fulani au msanii fulani kutokana na mambo yake lakini inapokuja kwenye muziki inakuwa tofauti maana msanii anapofanya wimbo mzuri, utajikuta tu unaimba wimbo ule kwa kuwa muziki una nguvu na haina mipaka, wala tofauti. Alikiba alizidi kusema kuwa hata kama unaweza kuwa unamchukia mtu inafika wakati unasahau na kupotezea na maisha ya kawaida yanaendelea na kujikuta ule utofauti wenu umepotea.

EATV

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here