Home Lifestyle Vanessa Mdee Hatimaye Aelezea Mbona Anapenda Kuvaa nusu utupu !

Vanessa Mdee Hatimaye Aelezea Mbona Anapenda Kuvaa nusu utupu !

Star huyu wa zamani wa Televisheni amesema kwamba anapenda kuvaa mavazi hayo ambayo hayakubaliki na  jamii kwa sababu anatangaza brand yake, ili kumwezesha kupata deal na Mafashionista mbalimbali duniani.Akiongea na kipindi cha  Friday Night Live kinachopeperushwa na East Africa Radio na EATV, Vee  aliongezea kwamba wasanii wengi wa kitanzania hawajajua na kutambua brand yao Jambo ambalo linawazuia kuteka anaga za kimataifa.

vanessa-mdee-tecno-own-the-stage

“Ukweli ni huu, wasanii for a long time in the past, wasanii wa kitanzania hawajajua na kutambua brand yao, mi brand yangu mi nataka ndani ya miaka miwili napigiwa simu na Balmain, na Lui V, nataka dersigners wakubwa wa dunia wanitumie kutangaza bidhaa yao kwa sababu wanaamini nina brand yangu kubwa na zinaendana, so nna malengo , na if im gonna offend any body im sory”, alisema Vanessa Mdee.

Utakumbuka kwamba ni juzi tu Vanessa Mdee aliiachilia Video yake Mpya ya Kaniroge ambayo inafanya vizuri sana , Jambo ambalo linatia matumaini yake ya kupandisha mziki wake katika ramani ya dunia hai.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here