Home Lifestyle VANESSA MDEE NA SHILOLE WAINGIA NDANI YA BIFU ZITO, SHISHI ATANGAZA VITA

VANESSA MDEE NA SHILOLE WAINGIA NDANI YA BIFU ZITO, SHISHI ATANGAZA VITA

Divas wa Bongo Flava, Vanessa Mdee na Shilole wameingia kwenye bifu zito.

Bado kisa na mkasa hakijabainika wazi lakini ni Shishi ndiye aliyeanza kumtupia maneno Vee Money kwenye Instagram. Kuna uwezekano mkubwa wawili hao walizinguana nyuma ya pazia kabla ya kuamua kuumwaga ubuyu mtandaoni. “Vee Jipange sana mwenzio Igunga niliaga sijaletwa kwa kubebwa kwenye lori, nimekuja na mbio za mwenge,” aliandika Shilole kwenye post ya Instagram ambayo imefutwa tayari. “We si wa magorofani na kiingereza chako cha kuunga, mi ndio mtoto wa mbwa sasa maninaa,” aliongeza Shilole.

Vanessa hakukaa kimya, alimjibu Shishi kwa post ambayo aliifuta muda mfupi baadaye. Akipost picha ya Shishi, Vee aliandika: Nikupe Kickiii ujulikane au sio? Kila siku twanyamaza ndio mtugaraze. Sit the f*ck down. Mimi sio wale uliowazoea. Ps: You ain’t worth this post inashushwa sasa hivi #MessageSent.” Haijashia hapo. Shilole amepost video akimpa ujumbe mwingine mkali zaidi muimbaji huyo wa ‘Niroge.’ “Vanessa nimepata ujumbe wako wa Kiingereza  japokuwa nimeusoma kwa tabu sana lakini nimepata baadhi baadhi,” anasikika akisema kwenye video hiyo. “Listen to me my sister, you see me nah, mimi mwenzio nimezaliwa Igunga, nimezoea kula ugali, sijazoea kula chips mayai kama unavyokula wewe. So mama ninapiga kuliko maelezo, usiombe kukutana na mimi, au waulize wenzio waliokutana na vibao vyangu wanaweza kukuambia kwamba kibao cha Shishi ukikutana nacho lazima uombe Panadol,” anaonya Shishi. “Aisee bibi, bibie, bibie, I am telling you yaani usiombe kukutana na Bi Shishi, yaani usiombe ukakutana na mimi tit for tat, yaani mama Kiingereza chako nimekiona, jipange, I am telling you, If I see you, me and you.” Acha tuone movie hii itaishia wapi. Lakini kwa vitisho hivyo Vanessa hana budi kuwa na bodyguard wake sasa.

Bongo5

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here