Mtangazaji maarufu wa Q Fm hapa nchini Kenya Rashid Abdalla amewasihi wasanii wote wa Kenya Kuambiana ukweli kuhusiana na hali ya muziki wa Kenya.
Wakijadili kuhusu muziki wa Kenya katika kipindi cha leo na munene Nyaga na Sameer Bry,Rashid ametaja kwamba wasanii wa kenya wanajuana,Wanajua nani mkali na nani hawezi ila hawataki kuambiana ukweli.
Kuhusiana na Watangazaji kupatia mziki wa Nigeria kipau mbele,Rashid amewaomba wasanii kufanya kazi bora na itakayokubalika badala ya kuwalaumu watangazaji an washika dau wengine.
Akichangia katika mada hiyo Sameer Bry amewaomba Wasanii kuiga mfano wa AY kutoka Tanzania ambaye amefanya bidii kutoa kazi tofauti na pia kuwekeza katika muziki.