Home Lifestyle “Wasanii Wengi Wanaendesha Magari Ya Kukodesha” – MSAMI

“Wasanii Wengi Wanaendesha Magari Ya Kukodesha” – MSAMI

Msanii wa bongo flava MSAMI ambaye kwa sasa anafanya poa na kazi yake mpya ‘Mabawa’ amefunguka na kusema kuna kundi kubwa la wasanii wa bongo fleva ambao wanaendesha magari ya showroom,Yani magari si ya kwao ndiyo maana kila siku wanabadili magari hayo sababu si ya kwao. Msami alikuwa akisema hayo kupitia kipindi cha eNEWS baada ya wiki hii kupata zawadi ya gari na kuonyesha kadi ya gari hilo, ndipo hapo aliposema kuwa yeye si kama wasanii wengine ambao wanatembelea magari ya watu, magari ambayo yapo kwenye biashara ndiyo maana hata ukiomba kadi ya gari wanazungusha sababu hawana kadi za magari hayo na yakiiuzwa wanapewa mengine ndiyo maana mara kwa mara wanabadili magari.
“Unajua mimi si kama hao wasanii wengine, mimi hii ni gari yangu ya nne kumiliki na ndiyo maana nakupa kadi ya gari yangu hii hapa sababu najiamini, nimeanza kumiliki gari kabla hata sijui kama nitakuwa msanii, hivyo hao wasanii watajua wenyewe siwezi kuwataja lakini uzuri hata nyinyi wenyewe mnawajua, uongozi wangu unafanyakazi kweli sababu wanatambua mimi si mtu feki feki naishi maisha yangu yenye uhalisia, ila wapo wasanii ambao wanaendesha magari ya showroom yakipata wateja wanapokonywa au kubadilishiwa mengine lakini hili ni langu” alisema Msami.

EATV

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here