Home Lifestyle WEMA Akanusha Kutaka Kurudiana na DIAMOND PLATNUMZ

WEMA Akanusha Kutaka Kurudiana na DIAMOND PLATNUMZ

Baada ya Wema Sepetu kupost picha katika mtandao wake wa instagram akiwahimiza watu kumpigia kura Diamond Platnumz katika tuzo za BET na kuibua mjadala mkubwa katika mitandao ya kijamii, malkia huyo wa filamu amefunguka mambo mengi. Mei 28 mwaka huu Wema alipost picha instagram na kuwataka watu kuwa wazalendo kwa kumpigia kura Diamond Platnumz katika tuzo za BET, lakini picha hiyo iliibua tetesi ya kwamba wawili ambao walikuwa wapenzi kipindi cha nyuma wanataka kurudiana huku mashabiki wengine wakiona kama muigizaji huyo anajitendekeza mbele ya staa huyo wa muziki.
Muigizaji huyo mahiri kupitia Global TV, amekanusha swala la kutaka kurudiana na Diamond huku akimtakia msanii huyo maisha mema na mpenzi wake wa sasa aitwae Zari.
“Mimi nataka waishi maisha mazuri yeye na mpenzi wake vizuri kwa raha na starehe, kwa sababu simwangalii tena Nasib kama mpenzi, alikuwa, namwangalia kama icon ya muziki, namwangalia kama mwanamuziki mzuri sana. Lakini siwezi hata leo sijui watu wanaseme tumerudia, mimi siwezi, kwa sababu ile hali ilishanitoka, kwa hiyo nimebaki namwangalia kama mtu ambaye anafanya vizuri kwenye muziki na ninamsifia,” alisema Wema.
Pia Wema alisema anatamani siku moja apatane na Diamond na waweze kuzungumza kama washkaji na kufanya biashara kwa pamoja.
“Na nnatamani, one day tuweze hata tuka kaa hivi tukaongea nikamwambia bwana embu tuondokane na mambo haya yote whatever it is me nitakusupport, wewe ukinisupport wala usiponisupport sababu yule naye mswahili sana”

Bongo5

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here