Home Lifestyle “Wema Sepetu Ndiye Aliyemaliza Pesa Ya Mshindi Wa Big Brother Idris Sultan”-...

“Wema Sepetu Ndiye Aliyemaliza Pesa Ya Mshindi Wa Big Brother Idris Sultan”- Adai Nay Wa Mitego

Rapper Mtukutu kutokea Manzese Nay Wa Mitego, amedai kuwa Fedha za Mtanzania mshindi wa Big Brother 2014 Idriss Sultan, zimefilisiwa na aliyekuwa Mpenzi wake Muigizaji Wema Sepetu.

Kupitia video fupi anazoweka kwenye mitandao ya kijamii, Rapa huyo amedai kuwa Idriss aliambiwa Mapema kabla hajafika Bongo kuhusiana na Wanawake waigizaji. “Huwa najiuliza kitu kimoja ni mwanamke gani amemaliza mahela ya Idris?,” aliuliza Nay kupitia video hiyo. “Ni yule Msouth au madam (Wema). Mimi nadhani atakuwa madam maana madamu ni mtu wakukwarua mahela mengi, tena kabla hajatua Tanzania walimwambi, huku nyumbani kuna wanawake wacheza sinema maharamia wakikukamata na hizo hela utajikuta huna hata mia,” Idriss Sultan alivuna kiasi cha Shilingi Milioni 500 za Kitanzania baada ya kushinda shindano hilo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here